Kiungo
wa timu ya Azam, Salum Abubakar amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba
wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja
mbalimbali nchini.
Abubakar
ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) aliwashinda
wachezaji wengine 20, huku wanne kati ya hao wakichuana naye kwa karibu.
Wachezaji
hao ni Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Rashid
Mandawa (Kagera Sugar) na Najim Magulu wa JKT Ruvu Stars.
Kwa
kuibuka mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha taslimu sh.
milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom.
Jopo
maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila
mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili
kumpata mshindi wa mwezi.







0 COMMENTS:
Post a Comment