CHEKA (KATIKATI) AKIWA NA WAANDISHI WA GAZETI LA CHAMPIONI, SALEH ALLY NA JOHN JOSEPH. |
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka ‘SMG’, ameibuka na
kusema kuwa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro ndiyo itaibuka bingwa wa
msimu huu wa Ligi Kuu Bara kutokana na ushindani inaouonyesha kwa timu
inazokutana nazo.
Mtibwa imeanza vizuri ligi kwa kuzifunga Yanga, Ndanda na Mgambo
JKT, kesho Jumamosi inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro
kuivaa Polisi Morogoro ambao wamekuwa wakiwasumbua kwa muda mrefu.
“Ndoto yangu ni kuona Mtibwa wanakuwa mabingwa wa msimu huu, kwani
naamini itakuwa ni zawadi kwetu watu wa Morogoro kwa sababu hata usajili wao
wameufanya kwa umakini mkubwa, ndiyo maana kila wanayekutana naye lazima
wamfunge,” alisema Cheka.
Mtibwa imekuwa ikishinda mfululizo tokea kuanza kwa ligi hiyo. Mechi yake ya kwanza iliyokuwa ya ufunguzi wa ligi ilitoa kipigo kwa
Yanga cha mabao 2-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment