BILO (KULIA) NA MUHIBU (KATIKATI) WAKIWA NA DAKTARI WA TIMU HIYO WAKIBURUDIKA NA GAZETI BORA LA MICHEZO NCHINI LA CHAMPIONI. |
Mkurugenzi wa Ufundi, Muhibu Kanu na Kocha Msaidizi Athuman Bilali
‘Bilo’ wa Stand United wameamua kurudi darasani kuongeza ujuzi kwa kusoma kozi
kupata leseni C ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).
Mkurugenzi huyo amesema kuwa wameamua kwenda kuongeza ujuzi ili kuwa
hodari zaidi katika kazi yao ya kufundisha kwa sababu wanataka kukiboresha
zaidi kikosi chao kiufundi.
“Tumeamua kwenda kusoma kuboresha mambo kadhaa katika benchi letu la
ufundi, mimi nitaanza hivi karibuni na kozi yangu nitachukulia mkoani Morogoro
na kocha ameshaanza kusoma yupo Dar es Salaam.
“Kocha mkuu yupo anaendelea kuinoa timu kama kawaida na kozi zenyewe
ni kwa muda mfupi tu, hivyo baada ya hapo tutarudi na kuendelea kuijenga timu
yetu kama kawaida,” alisema Kanu.
0 COMMENTS:
Post a Comment