HALL (KUSHOTO) WAKATI AKIWA BOSI WA AZAM FC. |
Mkurugenzi wa Symbion Sports na kocha wa
zamani wa Azam FC, Muingereza, Stewart Hall, ameipa nafasi timu Azam kuibuka na
pointi tatu katika mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine
mjini Mbeya.
Rekodi inaonyesha timu hizo zimekutana mara
mbili ambapo Mbeya City imetoka sare mechi moja na imepoteza moja.
Hall alisema kuwa Mbeya City msimu huu imekuja
kitofauti na msimu uliopita ambao walianza kwa kasi kubwa ndiyo maana walifanya
vizuri si kama sasa ingawa ligi ndiyo kwanza mwanzo.
Aidha alisema kuwa Azam bado wana kiwango
kizuri katika safu ya ushambuliaji na wamefunga mabao mengi.
“Si kwamba Mbeya City ni wabovu sana, hapana,
ila msimu huu hawako kama walivyoanza msimu uliopita, ndiyo maana naipa zaidi
nafasi Azam kufanya vyema katika mchezo wao wa leo ambao watakuwa ugenini
lakini matumaini makubwa ni ushindi.
“Azam katika eneo la ulinzi na
ushambuliaji wapo vizuri, ndiyo maana wana mabao mengi tofauti na wapinzani wao
ambao mpaka sasa mechi tatu bao moja pekee,” alisema Hall.
0 COMMENTS:
Post a Comment