MTIBWA SUGAR |
Timu za Mkoa wa Morogoro, Mtibwa Sugar na
Polisi Moro, leo zinatarajiwa kumenyana vikali kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara
katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Wakati homa ikipanda, Mtibwa imeshasema inahitaji
kushinda mechi sita mfululizo za mwanzo ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri
katika msimamo wa ligi kuu.
Mtibwa
mpaka sasa imeshinda mechi zake zote tatu ilizocheza na kufanikiwa kujikusanyia
pointi tisa mkononi.
Ofisa
Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amesema wamejipanga vyema kuhakikisha
wanaondoka na ushindi siku hiyo na lengo lao katika mzunguko wa kwanza ni
kuhakikisha wanashinda mechi sita za mwanzo.
“Tunahitaji kushinda mechi sita za mwanzo ili
kujikusanyia pointi nyingi na kuwa katika nafasi za juu kwenye ligi,” alisema
Kifaru.
0 COMMENTS:
Post a Comment