London, ENGLAND
UTAMU wa Ligi
Kuu England haushuki, maana kila wiki kuna kazi ya aina yake ambayo inakuwa na
burudani ndani yake.
Mechi za wiki
iliyopita zilikuwa zenye mvuto wa juu ukizingatia kulikuwa na mbili za watani
wa jadi.
Leo na kesho,
halikadhalika ni mechi ambazo si lahisi kujua ni nani ataibuka mshindi, mfano
zile za Sunderland dhidi ya Stoke City au Liverpool inayochechemea dhidi ya
wabishi Wes Brom, zote zitapigwa leo.
Kesho ndiyo
kibarua hasa,zitakazopigwa ni nne, lakini mbili Chelsea dhidi ya Arsenal na
Achana na Man
United wanaopambana na Everton, kila mmoja atatamani kukaa kwenye runinga na
kuangalia.
Wakati timu
zote zinashuka uwanjani, rekodi zinaonyesha kuna timu zenye rekodi nzuri
nyumbani, nyingi zina uwezo wa juu hata ugenini.
Timu hizo ndiyo
zinafanya ligi iwe na mvuto zaidi kwa kuwa zinaongeza ugumu na kuifanya isitabirike,
kwamba wakati wowote zinashinda tu bila ya kujali ziko ugenini.
Hizi hapa ni
timu tano zilizofanikiwa kuingia kwenye tano bora ya zilizoshinda nyumbani na
ugenini, au upande mmoja kati ya hiyo kutokana na ushindi au sare ilizozipata
katika mechi sita za Ligi Kuu England.
Chelsea:
Chelsea ndiyo
inaonekana iko vizuri zaidi, nyumbani au ugenini, inashinda tu. Imeshinda mechi
zake zote tatu za nyumbani na kubeba pointi tisa, halafu ikashinda mbili na
sare moja ugenini, haijapoteza kokote.
Southampton:
Southampton
imeshinda mechi mbili za nyumbani, sare moja, haijapoteza. Ugenini ikashinda
mbili pia na kupoteza moja tu. Hii inaonyesha ina kikosi imara pia, ila ‘pumzi’
yake kadiri ligi inavyosonga ndiyo itatoa majibu.
Man City:
City iko safi
pia, maana ugenini imeshinda mechi mbili katika tatu ilizocheza. Lakini mambo
si mazuri sana nyumbani kwa kuwa imechza naonyesha kuwa na kikosi imara pia,
katika mechi tatu za nyumbani, ina sare moja, imeshinda moja na kupoteza moja.
Aston Villa:
Wakali ugenini,
maama katika tatu, wameshinda mechi mbili. Ila nyumbani ndiyo mambo hayajaa
‘fresh’ maana wameshinda moja, sare moja na kupoteza moja. Hata hivyo si
wastani mbaya sana kwa kuanza.
Arsenal:
Nao wako vizuri
lakini si sana, katika mechi tatu za ugenini wameshinda moja na sare mbili,
maana yake hawajapoteza nje ya Emirates. Lakini waliporudi katika dimba la
kwao, wakashinda moja na kutoka sare mbili pia.
MSIMAMO WA NYUMBANI:
P W D L GF GA Pts
1 Chelsea 3 3 0 0 9 2 9
2 Southampton 3 2 1 0 6 1 7
3 Man
United 3 2 0 1 7 3 6
4 Swansea
City 3 2 0 1 4 1 6
5 Leicester
City 3 1 2 0 8 6 5
MSIMAMO WA UGENINI:
P W D L GF GA Pts
1 Chelsea 3 2 1 0 10 5 7
2 Man
City 3 2 1 0 8 4 7
3 Southampton 3 2 0 1 5 3 6
4 Aston
Villa 3 2 0 1 2 3 6
5 Arsenal 3 1 2 0 6 3 5
0 COMMENTS:
Post a Comment