MANYIKA (KATIKATI) AKISIKILIZA MAELEKEZO KUTOKA KWA KOCHA MZUNGU ALIYEKUWA AKIWANOA NCHINI AFRIKA KUSINI. ALIYEPIGA MAGOTI NI CASILLAS AMBAYE NI MAJERUHI. |
Pamoja na kutokuwa kwenye kikosi, Kocha wa Makipa wa Simba, Idd Pazi
‘Father’, amesema kuwa anaamini kipa kinda wa Simba, Peter Manyika akidaka
kwenye mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Yanga, atafanya vizuri.
Simba inakutana na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini, lakini
makipa wake chaguo la kwanza na la pili, wanaonekana kutokuwa fiti.
“Manyika ni kipa mzuri, kiwango chake kinaridhisha, sema tu kitu
kinachoweza kumfanya afanye vibaya ni presha kutoka kwa mashabiki, maana bado
mdogo. Ninaamini Manyika anaweza kukaa langoni bila shaka yoyote,” alifunguka
Father.
Pazi aliachwa kwenye safari ya Afrika Kusini ambako Simba ilikwenda
kuweka kambi.
Taarifa zinaeleza hakuwa na mkataba baada ya aliokuwa nao kwisha na
Simba ina mpango wa kuliimarisha benchi hilo la ufundi upande wa makipa.
0 COMMENTS:
Post a Comment