October 17, 2014



JOSHUA (KULIA) AKIWA MAZOEZINI JANA NA 'NGOZI' MPYA TAYARI KWA MECHI YA KESHO.

Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kushuka uwanjani kesho Jumamosi kupambana na wapinzani wao wa jadi, Simba, beki wa kushoto wa timu hiyo, Oscar Joshua, amenunua viatu vipya kwa ajili kukabiliana na washambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na Ramadhan Singano ‘Messi’.


Joshua, mwenyeji wa Mwanza, amefikia hatua hiyo kuhakikisha anawadhibiti vilivyo wachezaji hao ambao wanasifika kwa kuwa na kasi kali pindi wanapokuwa uwanjani.

Mchezaji wa Yanga ambaye amesema si ishu kubwa yeye kutajwa, amesema Joshua amewapania vilivyo wachezaji hao ambao wamekuwa chachu ya mabao ya Simba, kuhakikisha hawatengenezi nafasi yoyote ya kufunga katika mechi hiyo.

“Unajua hivi sasa kuna hali kama ya mvuamvua, hivyo ameamua kutafuta viatu vipya ambavyo vitamsaidia kutoteleza kila wakati pindi atakapokuwa akikabiliana na wachezaji hao.

“Okwi na Messi wanajulikana kwa kuwa na chenga za maudhi, hivyo kama mchezaji akiwa na viatu ambavyo meno yake siyo mazuri, wanaweza kumuaibisha na hilo ndilo lililomfanya Oscar afanye hivyo,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Baadaye SALEHJEMBE ilimshuhudia Joshua ndani ya viatu hivyo vipya na baadaye akathibitisha kweli ndiyo 'mzigo' huo mpya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic