Bosi wa benchi la ufundi la Yanga,Marcio Maximo,
amesema kuwa haiandai timu kwa ajili ya kuifunga Simba tu bali ni kwa timu zote
shiriki za Ligi Kuu Bara ili afanikishe malengo yake ya kutwaa ubingwa huo.
Yanga inakutana na Simba Oktoba 18, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ndiyo mchezo wao wa nne wa ligi.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa
kutokana na kila timu kutaka heshima huku kila moja ikijivunia usajili wake
ilioufanya msimu huu.
Lakini Maximo amesema wala haufikirii mchezo huo kabisa, zaidi anafanya maandalizi ya
kukiboresha kikosi chake kilichofungwa mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa Sugar huku
wakishinda mmoja na Prisons.
Maximo alisema, sera yake ni kuhakikisha
wanashinda kila mechi watakayocheza msimu huu ili kujiwekea mazingira mazuri ya
kutwaa ubingwa wa ligi kuu unaoshikiliwa na Azam FC inayofundishwa na Mcrameroon,
Joseph Omog.
“Naandaa
timu siyo kwa ajili ya Simba, isipokuwa kwa kila timu nitakayokutana nayo.
“Simba ni moja ya timu nitakazocheza nazo, hivyo
ninaendelea kukiandaa kikosi changu kwenye mazoezi yangu ya kila siku, hiyo mechi
ya Simba siifikirii kabisa,” alisema Maximo.
0 COMMENTS:
Post a Comment