Mshambuliaji mpya wa Simba, Elias Maguli,
amepewa majukumu ya kiungo mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera katika kipindi
chote atakachokaa nje ya uwanja.
Hiyo ni baada ya Kiongera kupata majeraha ya
goti wakati timu yake ilipocheza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya
Coastal Union baada ya kugongana na kipa wa timu hiyo, Shaaban Kado kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkenya huyo, awali kabla ya kuanza ligi kuu
alichaguliwa kuwa ‘super sub’ na kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia, Patrick
Phiri, anayekinoa kikosi hicho, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja miezi miwili
akiuguza majeraha ya goti.
Phiri
amesema kuwa majukumu aliyokuwa anayafanya Kiongera sasa amemkabidhi Maguli.
Phiri alisema, majukumu ya Maguli anayotakiwa
kuyafanya ni kuusoma mchezo wakati yupo benchi kabla ya kuingia kuubadili
akitokea nje ya uwanja kama ‘super sub’.
Aliongeza kuwa, anaendelea kumuandaa
mshambuliaji huyo kwenye mazoezi yake ili kuhakikisha anashika maelekezo
anayompa na kuyafanyia kazi kwenye mechi.
“Kabla ya Kiongera kupata majeraha ya goti,
nilikuwa namtumia kama ‘super sub’ kwa ajili ya kubadilisha mchezo akiwa nje
kwenye benchi langu.
“Nilifanikiwa kwa Kiongera kumbadilisha kutoka
kwenye kikosi changu cha kwanza na kumuandaa kuwa ‘super sub’ na ndivyo
nitakavyofanya kwa Maguli,” alisema Phiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment