Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Kassim Dewji leo amedondosha dua wakati mechi ya Ligi Bara kati ya Yanga dhidi ya Simba ikiendelea.
Dewji ambaye wakati wa uongozi wake Simba ilipata mafanikio makubwa, mara kadhaa alionekana akifumba macho na kuzungumza maneno kimyakimya.
Alifanya hivyo mara kadhaa mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ambaye alikuwa ametulia anafuatilia kwa ukaribu.
Mechi hiyo iliisha kwa sare, Simba wakicheza vizuri katika kipindi cha pili na Yanga wakiwapa wakati mgumu Simba katika kipindi cha pili.
Hata hivyo haikujulikana kama ndoto hizo pia zilikuwa ni kuomba sare kama ushindi ukishindikana...hehe....gwiji bana.
0 COMMENTS:
Post a Comment