Ndanda FC leo imeonja utamu wa kufungwa
nyumbani baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Ruvu Shooting.
Ndanda imefungwa mabao hayo ikiwa kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mabao ya Ruvu yalifungwa na Juma Ndeule,
Abrahman Mussa na Thomas Matayo.
Mjini Morogoro, Polisi Moro na Mtibwa Sugar zimemaliza dakika
90 bila ya kufungana.
0 COMMENTS:
Post a Comment