BAADHI YA MASHABIKI WA MBEYA CITY WAKIWA NA UZI ORIJINO WA MSIMU ULIOPITA. |
Klabu ya Mbeya City inayodhaminiwa na mabetri ya RB kutoka kampuni ya Bin Slum Tyres Ltd, imetangaza rasmi kuwa jezi zote za klabu hiyo zinazouzwa jijini Dar es Salaam ni feki.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amesema jezi za msimu mpya bado hazijatoka.
Lakini wamekuwa wakishanagzwa na wajanja wachache ambao wanauza jezi hizo hasa jijini Dar es Salaam.
UZI MPYA.... |
"Tunashangazwa sana na hawa watu wanaouza jezi feki za Mbeya City, wanajua wanafanya kosa lakini wanaendelea kufanya hivyo.
"Tuko katika mikakati ya kupambana na suala hilo na tunalipa uzito wa juu sana," alisema Kimbe.
"Jezi za msimu huu, zitatoka hivi punde, hivyo mashabiki wa Mbeya City wavute subira kidogo tu.
"Ila naweka msisitizo kwamba kununua jezi feki si kuiunga mkono klabu yao badala yake fedha zinakwenda mifukoni mwa wajanja wachache," alisema Kimbe.
Tayari Mbeya City imetangaza kuwa katika mikakati ya hatua za mwisho kufungua duka la vifaa katika jiji la Dar es Salaam ambalo pia litauza jezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment