October 1, 2014

BAADHI YA MASHABIKI WA YANGA AMBAO HUSHANGILIA KISTAARABU BILA YA VURUGU.

Mwenyekiti wa matawi ya klabu ya Yanga, Mohammed Msumi ametoa tamko la kuwataka wanachama wa Yanga kutulia ili kuiepusha klabu yao na matatizo.

Msumi amesema Wanayanga wanapaswa kuwa wanamichezo na kuiunga mkono Yanga katika kipindi kigumu badala ya kuzomea na kusababisha vurugu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msumi amesema wanaoonyesha jazba kisa Yanga imefungwa au kutoka sare, wanapaswa kujifikiria mara mbili.
“Angalia tumepigwa faini kutokana na vurugu za Morogoro baada ya kufungwa na Mtibwa Sugar.
“Shilingi laki tano ni nyingi, klabu ingeweza hata kununua maji kwa ajili ya wachezaji lakini si walivyofanya.
“Tukumbuke Yanga ni timu ya mpira, hauwezi kucheza bila ya kupoteza hata mechi moja na tunapaswa kuwa na busara,” alisema Msumi.
Yanga ilifungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Ku Bara.
Mechi hiyo ilionyesha kuwaudhi mashabiki hao waliokuwa wamesafiri kwa wingi kwenda mjini Morogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic