October 28, 2014


Uongozi wa Simba umetoa mechi mbili tu kwa Kocha Patrick Phiri kuhakikisha anafanya vizuri.

Akishindwa, huend anaweza kukabidhiwa mikoba yake na kwenda zake kwao Zambia.
Uamuzi huo wa Simba umefuatia kikosi chake kucheza mechi tano za Ligi Kuu Bara na kutoka sare zote.
Uongozi wa Simba lazima upambane kuhakikisha kuna matokeo mazuri, si jambo baya.
Lakini ni lazima kuwe na umakini mkubwa kwa kuwa wakati Phiri anapewa mechi mbili, uongozi wa Simba umesahau kuwa umechukua wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza ambao unawatuhumu kwa utovu wa nidhamu.
Maana yake wakati Phiri anaingia katika mechi yake ya kwanza ya kitimoto dhidi ya Mtibwa Sugar iliyo katika fomu, atawakosa Shabani Kisiga, Haruna Chanongo na Amri Kiemba.
Hata kama dharau itatangulia, kwanza tukubali ni wachezaji tegemeo na wawili kati ya hao wako kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Uzoefu wa Kisiga pia unahitajika ikizingatiwa Simba kwenye ushambuliaji haijakaa vizuri.
Hivyo kumpa Phiri mtihani, huku ikiondoa baadhi ya wachezaji si jambo sahihi.
Lakini bado inaendelea kuchanganya zaidi kwa kuwa Simba walipaswa kumpa kocha huyo nini cha kufanya baada ya kumalizana na wachezaji hao.
Kama wachezaji wamehujumu, vipi tena kocha awe kwenye presha kwamba asiposhinda yuko matatizoni.
Maana kama wachezaji wanahujumu, basi wao ndiyo tatizo, kama wao si tatizo sawa itakuwa ni kocha au viongozi.
Sahihi Simba ingefanya mambo kwa hatua, baada ya kumalizana na wachezaji hao watatu, ndiyo ingekwenda kwa kocha.
Kuyafanya yote kwa pamoja, pia inachanganya, maana yake haina uhakika kama tatizo ni wachezaji au kocha. Utafiti zaidi unaoendana na utulivu ulitakiwa katika hili.
Simba wasipokuwa makini wataongeza presha zaidi. Pia hawatakiwi kuiziingiza mechi zote 14 ambazo Phiri ameiongoza Simba.
Tisa ni za kirafiki na tano za ligi. Kwenye mechi za kirafiki, kocha anaweza kuweka wachezaji mchanganyiko kwa ajili ya kuangalia jambo.
Tathmini ya kutosha inapaswa zaidi kulenga kwenye mechi za ligi.
Bado utulivu unatakiwa katika utekelezaji wa mambo.
Kingine ni suala la uongozi wa Simba kuwazuia wajumbe wa kamati ya utendaji kuzungumza. Hakika ni jambo jema na itasaidia kupunguza na yasiyokuwepo.
Wako waliozungumza vizuri na kwa staha kubwa, lakini wako walionyesha si wanamichezo na uongozi wa Simba umefanya jambo sahihi kabisa.
TAKWIMU:
Amecheza 14, Ameshinda 4, Sare 7, amepoteza 3

TAKWIMU ZA MECHI ZA PHIRI NA SIMBA MSIMU HUU

Simba 2-1 Kilimani City (Kirafiki)

Simba 2-0 Mafunzo (Kirafiki)

Simba 5-0 KMKM (Kirarfiki)

Simba 3-0 Gor Mahia (Kirafiki)

Simba 0-1 URA (Kirafiki)

Simba  0-0 Ndanda (Kirafiki)

Simba 2-2 Coastal Union (Ligi Kuu Bara)

Simba 1-1 Polisi Moro (Ligi Kuu Bara)

Simba 1-1 Stand United (Ligi Kuu Bara)

Simba 0-0 Orlando Pirates (Kirafiki)

Simba 2-4-0 Bidvest Wits (Kirafiki)

Simba 0-2 Jomo Cosmos (Kirafiki)

Simba 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu Bara)


Simba 1-1 Prisons (Ligi Kuu Bara)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic