Kocha Patrick Phiri wa Simba amesema matokeo ya sare
mfululizo yanamuumiza sana.
Lakini akasisitia ndiyo wakati mwafaka ambao
Wanasimba wanapaswa kutulia na kutafuta jibu sahihi la tatizo.
“Hakuna anayefurahia haya matokeo, najua
mashabiki na viongozi wanaumia sana. Lakini makocha na wachezaji pia tunaumia.
“Hali si ya kawaida, lakini tunapaswa
kutulia badala ya kulumbana, tuangalie tatizo na mwisho tutafanya vizuri,”
alisema Phiri.
Simba imetoka sare tano mfululizo, hali
ambayo imezua zogo kubwa miongoni mwa Wanasimba.
Katika mechi zote tano ilizotoka sare, Simba
imetangulia kushinda halafu wapinzani wao wakasawazisha.







0 COMMENTS:
Post a Comment