Kocha wa zamani wa Simba, Talib Hilal ambaye
anafanya kazi zake nchini Oman amesema kuwa ni mapema sana kwa Simba kuanza
kulumbana sasa.
Hilal ambye pia aliichezea Simba akiwa mmoja
wa mabeki visiki, amesema Simba wanapaswa kukumbuka ligi ndiyo imeanza.
Katika mahojiano maalum na SALEHJEMBE, Hilal
amesema Simba ina kikosi chenye wachezaji wengi wapya.
“Wanahitaji muda, haraka haitawezekana hata
wafanyeje. Vizuri watumie muda mwingi kuwajenga kisaikolojia, natumai
hawatakuwa na tatizo la kiufundi kubwa.
“Lakini vizuri pia kumpa kocha nafasi,
lazima wakumbuke ana muda gani tokea amechukua timu hiyo mpya.
“Kingine waangalie wana majeruhi kadhaa
wamejitokeza, hivyo wajue lazima kuna upungufu unatokea na lazima ushughulikiwe
kwa kufuata utaratibu mzuri,” alisema ambaye ni Kocha wa timu ya taifa ya ufukweni ya Oman.
Hilal ndiye aliipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu
Bara (ligi ndogo) mwaka 2008, kikosi chake kikiishinda Yanga ya Sredojevic
Milutin ‘Micho’.







0 COMMENTS:
Post a Comment