Beki Gerard Pique wa Barcelona na timu ya
taifa ya Hispania, amewatolea lugha kali Polisi wa Usalama Barabarani baada ya kumlamba faini ndugu yake.
Pique alifanya hivyo wakati akirejea
Hispania baada ya kuitumikia timu yake ya taifa kwenye michuano ya kimataifa.
Ndugu yake aitwaye Marc ndiye alipaki gari
kwa dakika 15 katika eneo la mabasi na kusababisha usumbufu.
Pique ambaye ni mzazi mwenza wa mwanamuziki
maarufu, Shakila alipinga hilo na kuanza kuwasukumbia maneno makali polisi hao.
“Mnanipiga faini bila sababu, au kwa kuwa
mnaniona mimi ni maarufu.
“Mnafanya hivyo kusudi mpate fedha za
pongezi, ngoja, nitazungumza na mabosi wenu, nyie ni dhuluma tu,” alisema
akionyesha kuwa na jazba.
Hata hivyo, baadaye, Pique alilazimika
kuomba radhi kutokana na kitendo hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment