Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham ya England
ambaye sasa anakipiga Santos ya Brazil amejikuta akiingia matatani baada ya
kujivuta jezi na kuanguka.
Leandro Damiao alijivuta jezi na
kuanguka wakati akiichezea Santos katika Ligi ya Brazil.
Damiao alifanya hivyo akiwa katika harakati
za kumshawishi mwamuzi.
Hata hivyo mwamuzi huyo alishitukia mchezo,
hakutoa adhabu hiyo ya penati.
Tayari Shirikisho la Soka la Brazil (CBF)
liko katika hatua za kumchukulia hatua na imeelezwa adhabu yake huenda ikawa ni
kufungiwa kucheza mechi sita za ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment