October 2, 2014


Udhamini wa Kampuni ya kuuza matairi na betri ya Bin Slum Ltd, umeendelea kuiongezea neema Mbeya Cuty.
Kwani kampuni ya vinjwani baridi ya Coca Cola, imemwaga milioni 150 kwa Mbeya City.



Bin Slum ndiyo wadhamini wakuu wa Mbeya City kupitia bidhaa yake ya betri za magari za RB.
Hali hiyo inaonekana kuwavuta wadhamini wengine kujitokeza kuidhamini timu hiyo.

Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amethibitisha hilo kwa kusema mkataba huo ni wa miaka miwili.
"Kila msimu mmoja Coca Cola itatoa shilingi milioni sabini na tano.
"Pia wanatudhamini katika suala la vinywaji baridi, kitu ambacho tunakichukulia ni jambo jema kupata udhamini huo," alisema Kimbe.
Msimu uliopita, Mbeya City ilishika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara ukiwa ndiyo msimu wake wa kwanza kupanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic