Ronaldo ndiye mshambuliaji mwenye kasi zaidi ya kupachika mabao
kwa maana ya wastani.
Hadi sasa ana wastani wa kufunga bao katika kila dakika 42
alizoichezea Real Madrid kwenye la Liga.
Anafuatiwa na Neymar ambaye amecheza msimu mmoja wa La Liga na huu
ni wa pili akiwa na Barcelona.
Neymar ana wastani wa kufunga bao katika kila dakika 52
alizoichezea Barca.
Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi anaonekana kutokuwa
na bahati ya kutosha.
Kwani ana wastani wa dakika 102 ili kupata bao moja.
Maana yake hana uhakika wa kupata bao katika dakika 90 za mchezo
mmoja. Anaweza kufunga au la.
Tayari wachambuzi wa soka nchini Hispania wanaeleza huenda Messi
atakuwa na mabao kiduchu zaidi, lakini atafanya vizuri zaidi kwenye pasi
zinazozaa mabao yaani asisti.
0 COMMENTS:
Post a Comment