October 5, 2014


Penzi la beki wa Barcelona, Gerard Pique na mwanamuziki maarufu Shakira linazidi kupamba moto.
Ingawa hivi karibuni amekuwa akisakamwa kwa kuwa mara nyingi anaonekana na mzazi mwenzake huyo.

Pique amekuwa hajali masuala hayo, badala yake ameamua kuwa mtu wa familia zaidi.
Mara baada ya Barcelona kushinda mechi yake ya La Liga dhidi ya Rayo ambayo waliitungua mabao 2-0, akamchukua ‘bebi’ wake Shakira, kwenda kuchuma uyoga.
Pique, Shakira na rafiki zao kadhaa walikwenda kijijini kusaka sehemu kunakopatikana uyoga.

Walipofanikiwa kuupata, waliona wenye furaha, wakapiga picha na kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii wakionyesha kutojali maneno ya watu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic