November 8, 2014


Mshambuliaji Kun Aguero ameiokoa mara mbili Man City ambayo imenusurika kuzama ugenini katika mchezo wa Ligii England, leo.

QPR waliokuwa wenye wa mabingwa hao watetezi wa England, walianza kufunga, Kun akasawazisha, wakafunga la pili, akasawazisha tena.

Charlie Austin aliifungia QPR bao katika dakika ya 21 lakini Aguero akasawazisha katika dakika ya 32 na mabao hayo yakadumu katika kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili, beki wa City, Demichelis akajifunga la pili wakati akijaribu kuokoa lakini Aguero tena akasawazisha katika dakika ya 83 baada ya kupokea pasi ndefu ya Yaya Toure.

QPR:
Green, Isla, Caulker, Dunne, Yun, Vargas, Sandro, Henry, Fer, Austin, Zamora.
Subs: Hill, Phillips, Barton, McCarthy, Onuoha, Kranjcar, Hoilett.
Man City:
 Hart, Sagna, Demichelis, Mangala, Clichy, Fernandinho, Fernando, Jesus Navas, Toure, Nasri, Aguero.
Subs: Zabaleta, Milner, Dzeko, Caballero, Lampard, Jovetic, Boyata.

Referee: Mike Dean (Wirral).


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic