Mtibwa Sugar
na Kagera Sugar, leo zimemalizia kiporo chao cha pili kwa kutoka sare ya bao
1-1.
Kama unakumbuka
jana mchezo ulivunjika wakati Mtibwa Sugar ikiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa
na Ame Ali.
Lakini mvua
kubwa ikalazimu pambano liahirishwe na leo asubuhi kwenye uwanja wa Manungu,
dakika 45 zilizobaki zikamaliziwa.
Kagera
ikapata bao lake kusawazisha kupitia kwa Rashidi Mandawa katika dakika ya 57.
Sare hiyo ni
ya tatu kwa Mtibwa Sugar ambayo imeshinda mara nne na kuendelea kubaki
kileleni.
0 COMMENTS:
Post a Comment