Kocha Mkuu wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amedai
kubaki njia panda baada ya kiungo wake, Luka Modric kuumia akiwa na kikosi cha
timu ya taifa ya Croatia.
Modric anaweza kuwa nje ya uwanja mpaka
Januari mwakani, lakini kiungo wa kimataifa wa Hispania, Isco anatarajiwa kuwa
mbadala wake.
Japokuwa timu hiyo pia ina viungo Wajerumani,
Sami Khedira na Toni Kroos, lakini Ancelotti ameonekana kumkubali zaidi Modric
ambaye amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu kila siku.
"Khedira na Kroos ni pacha walioshinda
Kombe la Dunia, lakini nimepanga kujaribu kuwatumia Isco na Kroos kwa kuwa ninaamini
hawa wanaweza kucheza vizuri hasa katika kuilinda timu,” alisema bosi huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment