November 22, 2014


Mshambulia Olivier Giroud wa Arsenal, anaweza kucheza Arsenal itakapokuwa na kibarua kigumu dhidi ya Mashetani Manchester United kwenye mchezo wa Premier League katika Uwanja wa Emirates jijini London, leo.


Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 28, alikuwa nje ya uwanja tangu Agosti, mwaka huu alipoumia goti wakati wa mchezo dhidi ya Everton.

"Giroud amewahi kwa wiki tatu au nne, awali tulipanga tuwe naye kwa ajili ya mashindano mwanzoni mwa mwakani, kwa hiyo amewahi kwa mwezi mmoja kabla,” alisema Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.


Wenger pia alithibitisha kiungo wake, Mikel Arteta, 32, aliyekuwa ameumia mkono katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Anderlecht ulioisha kwa sare ya mabao 3-3, pia amerejea katika timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic