November 10, 2014


Mshambuliaji mkongwe wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba, ataendelea kula shavu katika klabu hiyo baada ya uongozi kudai kuwa bado unamhitaji, licha ya kutomtumia mara kwa mara katika mechi za Ligi Kuu Bara.


Mwaikimba ni miongoni mwa wachezaji wakongwe kwenye Ligi Kuu Bara. Aliwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa, Tanzania Prisons, Moro United na Ashanti. Amecheza ligi hiyo zaidi ya misimu 10.

Mwaikimba amebakiza mkataba wa miezi sita Azam FC na anaweza kufanya mazungumzo na klabu yoyote lakini Azam imesema haitaki kumuacha.

Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassor, amesema bado wanamhitaji mtupia kambani huyo.

“Mwaikimba bado ni mchezaji wetu na ana mkataba na Azam, hivyo hatuwezi kumzungumzia sana kwa sasa ila bado tunamhitaji na ataendelea kuwa mchezaji wa Azam,” alisema Nassor.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic