Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Mlage
Kabange, amelazimika kuiacha timu hiyo kwa muda kufuatia kurudi darasani kwa
ajili ya kujiendeleza kielimu.
Kagera Sugar ambayo inanolewa na kocha
mkuu, Jackson Mayanja wa Kenya, imedumu na Kabange kwa muda mrefu na makocha
wengi wamekuwa wakija na kuondoka huku wakimuacha Kabange.
Kabange amesema amelazimika kuachana
na timu hiyo kwa muda kwa ajili ya kurudi darasani katika kujiendeleza na masuala
ya ukocha mkoani Morogoro.
“Nipo mkoani Morogoro kwenye kozi fupi
ya ukocha ya wiki mbili na timu nimeiacha na kocha Mayanja, hivyo nitarudi
baada ya kumaliza kozi yangu.
“Lengo langu ni kuendeleza elimu yangu
ili nikirudi niweze kuwa bora zaidi, kuhusu ligi ni ngumu kwa kuwa kila timu
imejipanga ipasavyo kuhakikisha inashinda na kusonga mbele,” alisema Kabange.
0 COMMENTS:
Post a Comment