Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wameamka na kuichapa Coastal Union kwa mabao 2-1.
Katika mechi iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, Dar es Salaam, mabao yote yalifungwa katika dakika tano za mwisho.
Bao la kwanza la Azam FC lilfungwa katika dakika ya 84 kupitia Kipre Herman Tchetche.
Wakati Coastal wakiendelea kupambana kusawazisha, beki Shomari Kapombe alifunga bao la pili katika dakika ya 88 baada ya kuwapita mabeki wa Coastal Union na kupiga shuti lililomshinda Shabani Kado.
Lakini Coastal hawakukata tamaa baada ya kupata bao la kufutia machozi katika dakika ya 90 likifungwa na Rama Salim kwa mkwaju wa mpira 'uliokufa'.
0 COMMENTS:
Post a Comment