November 8, 2014


Pamoja na kuonyesha soka safi, Mgambo Shooting ya Tanga imeshindwa kuhimili mikiki ya Yanga na kukubali kipigo cha mabao 2-0.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga walipata mabao yao yote kupitia kwa Simon Msuva katika dakika ya 73 na 90.
Kabla ya mechi hiyo, Yanga ilikuwa imepoteza mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Licha ya kumkosa nahodha wake, Nadir Haroub 'Cannavaro', Yanga ilionyesha soka safi huku soka lake likiwa ni la kuvutia.
Mgambo nao walikuwa wakipeleka mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga lakini hawakuwa makini kwenye umaliziaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic