OMOG AKIWA NA MSAIDIZI WAKE KALLY ONGALLA AMBAYE SASA AMEKWENDA MASOMONI. |
Siku chache baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Azam FC, kumsainisha beki
Muaivory Coast, Serge Wawa, wamezidi kuvalia njuga suala la kuimarisha kikosi
chao katika usajili wa dirisha dogo, ambapo wameahidi kuongeza kifaa.
Azam
ambao walitwaa ubingwa kwa rekodi ya kutopoteza mchezo wowote, msimu huu
wameonekana kuyumba, huku wakiwa tayari wamepoteza mechi tatu, ukiwemo wa Ngao
ya Jamii, jambo ambalo limewalazimu kuimarisha kikosi zaidi.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog, alisema
katika ripoti yake aliainisha baadhi ya vitu ikiwemo suala la kuandaa mapema
programu za mazoezi wiki moja baadaye pamoja na kuimarisha baadhi ya safu.
Hata
hivyo, amesema kuwa baada ya Wawa, ndani ya wiki mbili kuna mchezaji anaweza
kutua Chamazi, japo hakutaka kuweka bayana wasifu wake.
“Kuhusu
usajili, kuna watu tunawahitaji lakini hilo siwezi kusema ni nani na anatoka
wapi, inabaki siri yetu,” alisema Omog.
Kama atakuwa ni mchezaji wa ndani, basi kwa asilimia kubwa atakuwa ni Amri Kiemba wa Simba ambaye tayari uongozi
wa Simba umethibitisha kupata barua ya maombi kutoka kwa Azam wakimtaka kwa
mkopo.
0 COMMENTS:
Post a Comment