MHANDO AKIZUNGUMZA NA MAMA MMOJA WA MASHABIKI WA CHINA WALIOKUWA UWANJANI. |
Mmoja wa wadau wakubwa wa
blog ya SALEHJEMBE ni Evans Mhando. Wengine wanamkumbuka wakati akipiga kazi
pale TBC.
Sasa Mhando yuko masomoni
nchini China na jana alijitokeza kucheki mechi kati ya wenyeji na New Zealand.
Mechi hiyo ya kimataifa
iliisha kwa sare ya 0-0. Mhando alikuwa mmoja ya waliokuwa uwanjani na akasema
alipata funzo kubwa.
“Tofauti na nyumbani, hapa
kwenye mechi nimeona wasichana wadogo, kina dada, kina mama na hata kina bibi
kwa wingi sana.
“Tofauti na nyumbani na hii
inatokana na kwamba, wenzetu hawana tabia mbaya za kutukana matusi.
“Uwanjani inaonekana suala
la matusi ni kawaida, hivyo linawakimbiza wanawake wengi na hasa watu wazima. Inabidi
tubadilike, kwa kweli nimepata funzo kubwa,” anasema Mhando.
Yeye amejifunza, kawa wazi
amewapasia wasomaji wa blog hii, kazi kwenu.
0 COMMENTS:
Post a Comment