November 2, 2014


 
Man City imeshinda bao 1-0 dhidi ya Manchester United katika mechi iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa nchini England na duniani kote.

Mechi hiyo iliyokuwa ‘tamu’ na yenye ushindani mkubwa imeisha kwa wenyeji hao kuibuka na ushindi huo baada ya Sergio Aguero kufunga bao katika dakika ya 63.
Aguero raia wa Argentina aliunganisha krosh kutoka kushoto ya Gael Clichy baada ya mabeki wa United kumsahau.

Man United licha ya kuwa pungufu baada ya beki wake Chris Smalling kulambwa kadi nyekundu ilijitahidi kusawazisha lakini wapi bana!
Smalling alilambwa kadi ya njano ya pili iliyozaa nyekundu katika dakika ya 39.










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic