Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Mlage Kabange amejivunia
ubora wa bao lililofungwa na mshambuliaji wake Paul Ngwai katika mechi dhidi ya
Yanga.
Yanga ililala kwa bao 1-0 katika mechi hiyo dhidi ya
Kagera ikiwa nyumbani Kaitaba mjini Bukoba, jana.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Kabange alisema bao alilofunga
Ngwai linawafanya Yanga wasiwe na cha kulalama.
Ngwai alifunga bao hilo ukiwa ndiyo mpira wake wa kwanza anaugusa baada ya kuingia. Krosi ya juu ambayo aliunganisha moja kwa moja na kumuacha Deo Munishi 'Dida' akiduwaa.
“Ni bao bora kabisa ambalo halina ubishi, bao kama yale
ambayo unaweza kuyaona Ulaya.
“Hilo litakuwa moja ya mabao bora kabisa na utakubaliana
na mimi kama uliliona,” alisema kocha huyo.
“Kwa kweli tiliyafanyia kazi makosa ya mechi zilizopita,
halafu tukawa tayari kwa ajili ya Yanga na kweli umeona soka letu.
“Yanga walicheza vizuri, huenda hawakuwa pia na bahati
lakini hii ilikuwa siku yetu.”







0 COMMENTS:
Post a Comment