Wakati harakati za usajili kwa timu za
Ligi Kuu Bara zikizidi kushika kasi, mambo yanaonekana kumwendea vibaya kipa wa
Simba, Hussein Shariff ‘Casillas’ ambaye muda wowote anaweza kufungashiwa
virago vyake klabuni hapo.
Kipa huyo ambaye alijiunga na Simba
hivi karibuni akitokea Mtibwa, tangu atue klabuni hapo, ameshindwa kuonyesha
ubora wake wa msimu uliopita uliomfanya atwae tuzo ya kipa bora wa ligi kuu
msimu huo.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza uongozi unaangalia uwezekano wa kuachana na kipa huyo kutokana na kushindwa kuonyesha
makali yake katika mechi chache alizoitumikia, kabla ya kuumia mguu.
Pia hofu ya kuwa majeruhi inawapa hofu, ingawa anaweza akabaki kama Simba haitaongeza kipa mwingine.
“Ukiachana na kiwango lakini pia kuna
mambo ambayo amekuwa akiyafanya ambayo yamekuwa hayawapendezi viongozi pamoja
na baadhi ya wachezaji wenzake.
“Hivi sasa Casillas hazungumzi na Ivo
Mapunda, sababu kubwa iliyosababisha wafikie hali hiyo ni mambo ya ushirikina,
kila mmoja anamtuhumu mwenzake, jambo ambalo linaweza kusababisha balaa katika
kikosi chetu.
“Kutokana na hali hiyo uongozi umeona
ni bora uachane na Casillas ili kuepusha matatizo zaidi ambayo yanaweza
kujitokeza hapo baadaye endapo ataendelea kubakia klabuni hapo,” kilisema
chanzo hicho cha habari.
Ofisa Habari wa Simba, Humphrey
Nyansio alipoulizwa juu ya mpango huo wa kutaka kumfungashia virago Casillas,
hakuwa tayari kuzungumza lolote juu ya suala hilo zaidi ya kusema: “Sijapata
taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment