Mshambuliaji wa Yanga, Mbrazil, Geilson Santos ‘Jaja’ aliwaaga wachezaji wake
kabla ya kurudi kwao Brazili kwa kuwaambia kwamba hatarejea tena kuichezea
Jangwani mara atakaporudi kwao, imefahamika.
Hiyo ni siku
chache tangu uongozi wa Yanga utangaze kumuacha mshambuliaji huyo na kumsajili
mwingine Mbrazili, Emerson De Oliveira, 24, anayetarajiwa kutua nchini kesho Jumanne
akiongozana na kocha wake, Marcio Maximo.
Mshambuliaji
huyo, amefanikiwa kufunga bao moja pekee katika Ligi Kuu Bara akicheza michezo
yote saba ambalo alilifunga wakati timu yake ilipocheza na Stand United kwenye
Uwanja wa Kambarage.
Kwa mujibu wa
rafiki wa karibu wa mshambuliaji huyo, taarifa za kuondoka kwa Jaja hazijawashtua
kabisa wachezaji kutokana na kuaga kutorejea kuichezea tena Yanga mara
atakaporejea kwao Brazil.
“Hizo taarifa za
kutorejea kwa Jaja, mimi hazijanishtua kabisa kwa sababu kabla ya kuondoka
niliwahi kukaa naye na kuniambia kuwa, mara atakaporejea kwao basi hatarudi
tena kuichezea Yanga.
“Siyo mimi peke
yangu kuniaga, wapo baadhi ya wachezaji ambao alikuwa nao karibu aliwaaga na
sababu kubwa ikiwa ni mashabiki kuonekana kutokubali uwezo wake.
“Mashabiki
walikuwa wakimpa presha akiwa ndani na nje uwanja, amekuwa akikosa amani kabisa
hali iliyomfanya ashindwe kucheza soka, hivyo akaona ni bora asirudi tena na
badala yake aende akatafute maisha kwingine,” kilisema chanzo hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment