Mshambuliaji Mnigeria, Emeh Godwill Izuchukwu,
amesema anataka kurejea Simba na kuendelea kuichezea huku akiahidi mabeki Ligi
Kuu Bara watayaona maajabu yake.
Mshambuliaji huyo wa zamani, sasa anakipiga
katika timu ya daraja la pili ya Elverum FC ya nchini Norway.
Izuchukwu, raia wa Nigeria, tayari amepiga
simu nchini na kuwasiliana na mmoja wa rafiki zake ambaye ni mwanasheria ambaye
inaelezwa amewasiliana na viongozi wa Simba akitaka kurejea nchini.
Hata hivyo, uongozi wa Simba bado haujatoa
msimamo ingawa inaelezwa huenda akarejeshwa kuongeza nguvu kwenye safu ya
ushambuliaji.
Izuchukwu anaweza kurejeshwa kwenye dirisha
dogo la usajili linalofunguliwa Jumamosi ijayo.
Mnigeria huyo akiwa na Mnigeria mwenzake, Orji
Obina waliichezea Simba miaka minne iliyopita na kuwa miongoni mwa
washambuliaji hatari.
Hata hivyo, aliondoka nchini kwenda Sweden
ambako alijiunga na Klabu ya Enkoping na baadaye Assyriska FC kabla ya kuondoka
Sweden na kutua Ranheim IL ya Norway.
Phiri, Poulsen wapanga mabegi Dar, Denmark
Poulsen apanga mabegi Denmark, Phiri apanga
Dar
Na Ezekiel Kitula
MAKOCHA Patrick Phiri na Kim Poulsen, kila
mmoja ameanza kupanga mabeki kwa wakati wake kwa malengo tofauti.
Phiri anajiandaa kuondoka Simba kwenda likizo
kwao Zambia baada ya Ligi Kuu Bara kusimama huku akiwa ameiongoza Simba
kushinda mechi moja kati ya saba.
Lakini Poulsen ambaye amefanya mazungumzo na
Simba, anapanga mabegi yake kujiandaa kutua nchini wakati wowote kuchukua
nafasi ya Phiri ambaye inaelezwa hatarejea tena nchini.
Ligi itaendelea tena Desemba 26, baada ya
kusimama rasmi jana.
Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa
kuna mkanganyiko katika jambo hilo kuhusiana na Phiri na Poulsen.
“Kidogo linachanganya, lakini Phiri akiondoka,
sidhani kama atarejea, ni suala la kujua baadaye. Lakini Poulsen pia yuko
tayari kuja,” chanzo kilieleza.
Simba imeamua kuongeza nguvu na kufanya
marekebisho kwenye benchi la ufundi kwa kumleta Poulsen aliyewahi kuinoa Taifa
Stars.
Lakini kuna baadhi ya wajumbe wa kamati ya
utendaji wameonyesha kutofurahishwa na jambo hilo huku wakisisitiza Phiri
aendelee kubaki.
Kisiga in, Kiemba, Chanongo out
Kiemba, Chanongo bye bye Simba
#Kisiga arudishwa
Sweetbert Lukonge na Wilbert Molandi
BAADA ya mchakato wa kuchanganua mambo, kuna
asilimia kubwa Kamati ya Utendaji ya Simba ikatoa majibu ya kuwaondoa wachezaji
wawili, Amri Kiemba na Haruna Chanongo.
Lakini kiungo mkongwe, Shabani Kisiga anapewa
nafasi ya kuendelea kuitumikia timu hiyo kutokana na utetezi wake.
Watatu hao walisimamishwa kwa tuhuma za utovu
wa nidhamu na kucheza chini ya kiwango na baadaye wakaonyesha utovu wa nidhamu
kwa kushindwa kutokea kwenye kikao cha viongozi.
“Wachezaji walivyojieleza, inaonekana Kisiga
amekuwa hana matatizo makubwa na hata imefikia kwamba atasamehewa.
“Lakini Kiemba na Chanongo, kuna zaidi ya
asilimia tisini wataondoka Simba. Sijui, labda mambo yabadilike tena mwishoni,
si unajua uongozi ni kitu cha watu wengi,” kilieleza chanzo.
“Watu wengi hawajui uongozi unafanya nini, ukweli
ni kwamba uongozi unajua kila kitu, unajua mambo mengi kuliko watu wanavyojua
na wala hauna nia ya kumuonea mtu, lengo kuisaidia timu.”
Uongozi wa Simba, bado haujatangaza lolote
kuhusiana na hilo lakini utakuwa na nafasi ya kumalizia uamuzi huo na
kuutangaza ndani ya wiki hii.
Mara baada ya mchezo wa jana ambao Simba
walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi Ruvu Shooting, Kisiga pekee ndiye alishuka
chini baada ya mchezo kumalizika na kwenda kuwapongeza wachezaji wenzake
vyumbani.
Hata hivyo, kocha wa Simba, Patrick Phiri,
alipoulizwa kama suala lake limekwisha, alisema waulizwe viongozi.
Fin.
Mwadui, Villa zatesa daraja la kwanza
Nasor Gallu na Alpha Amos
TIMU ya Villa Squad ya Dar es Salaam na Mwadui
ya Shinyanga, jana zilifanikiwa kushinda mechi zao za Ligi Dara la Kwanza.
Villa inayonolewa na kocha Habib Kondo,
ilifanikiwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya African Lyon katika mtanange uliopigwa
Uwanja wa Karume. Mabao ya Villa yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba
na Yanga, Pius Kisambale dakika ya 19 na 87 huku la Lyon likiwekwa kimiani na
Omari Ramadhani dakika ya 72.
Nayo Mwadui inayonolewa na kocha Jamhuri Kihwelo
‘Julio’, iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa Green Warriors kwa
mabao 2-0 kwenye Dimba la Mwadui, Shinyanga.
Mabao ya Mwadui yalifungwa na Bakari Kigodeko dakika ya nane na Said
Sued dakika ya 17.
0 COMMENTS:
Post a Comment