Michuano ya Cecafa Senior Chalenji
sasa haipo tena baada ya waandaaji Ethiopia kujitoa, hivyo kukosa muandaaji
mbadala.
Michuano hiyo ilitarajiwa kuanza
Novemba 24 hadi Desemba 9, mwaka huu huko Ethiopia bingwa mtetezi akiwa ni
Kenya.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya
Soka vya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Nicholas Musonye, alisema baada ya
Ethiopia kujitoa, imekuwa ngumu kupata nchi mbadala ya kuandaa michuano kwa
haraka.
“Hatukupenda, lakini imeshindikana
kabisa, tulifanya kila juhudi lakini mambo yamekuwa ni magumu,” alisema
Musonye.
Alisema imekuwa ngumu kupata wadhamini pia kwani waandaaji walijitoa
dakika za mwisho, hali iliyowachanganya.
0 COMMENTS:
Post a Comment