Rais wa Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amesema baba yake mzazi ndiye alisababisha
awe shabiki wa Yanga.
Kikwete ameyasema hayo
katika mahojiano yaliyorushwa na E FM jana na kusema alipomuona baba yake
akiishangilia Yanga, naye akamfuata.
“Baba yangu alikuwa ni
Yanga, basi na mimi nikaamua kuwa Yanga na kuanzia siku hiyo nimekuwa nikiiunga
mkono.
“Kwa nje ya Tanzania mimi
ni shabiki wa Newcastle ya England. Aliyenivutia kuanza kuishabikia ni Alan
Shearer.
“Wakati naanza kuishangilia Newcastle kilikuwa ni kipindi
ambacho Shearer anatamba sana,” alisema Kikwete na kuongeza:
“Kwa watoto wangu wako huru
kushangilia timu wanazozitaka. Mfano kwa nje ya Tanzania, wako wanaoshangilia
Liverpool, Manchester United na Chelsea, hivyo niko pekee ninayeishangilia
Newcastle.”
Kikwete ndiye rais
mwanamichezo zaidi wa Tanzania katika awamu zote nne za uongozi nchini.
Ndiye rais pekee ambaye
alichukua uamuzi wa kutoa fedha kumlipa kocha wa timu ya soka ya taifa, Taifa
Stars.
0 COMMENTS:
Post a Comment