November 5, 2014


Simba imeamua kufanya mabadiliko tena katika benchi la ufundi na nguvu zimeelekezwa kwa Kocha Mdenishi,  Kim Poulsen.

Poulsen raia wa Denmark katika nafasi ya Mzambia Patrick Phiri ambaye timu yake imecheza mechi sita mfululizo na kutoka sare zote.
Simba imeingia kwenye harakati za kumng’oa Phiri ambaye ameingoza Simba katika mechi sita tu za Ligi Kuu Bara na zote ametoka sare. Simba imefunga mabao sita, imefungwa sita na ina pointi sita.
Mdenishi Poulsen ambaye yuko kwao nchini Denmark baada ya kuzinoa timu za taifa za vijana na baadaye Taifa Stars, aliondolewa kwenye kiti chake baada ya kuingia kwa uongozi wa Jama Malinzi.
Habari za uhakika za uhakika ambacho Championi Jumatano imezipata ni kuwa Simba wamefanya mazungumzo na Poulsen na kukubaliana kila kitu na yuko tayari kucha nchini wakati wowote.
Lakini kumekuwa na suala la Phiri kidogo limekuwa likiwagawanya kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji kutaka apewe mechi ya mwisho ambayo itakuwa ni dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili.
“Kweli viongozi wamejadili kila kitu na Poulsen, ni uhakika kama ulivyosema. Wamekubaliana suala la mshahara na kila kitu kipo wazi.
“Poulsen amewaeleza mshahara, mwisho wamekubaliana. Halafu likafuatia suala la nyumba, kocha amesema angependa kuishi Masaki, pia wamekubaliana katika hilo.
“Mwisho lilikuwa ni suala la usafiri na tiketi za kwenda na kurudi kwao Denmark, hilo pia wamekubaliana. Hivyo wanachosubiri huenda kikawa ni mechi ya Jumamosi na kama si mechi hiyo, basi angekuwa ameishatua,” kilifafanua chanzo.
“Ila hata hivyo inachanganya, kama Simba ikishinda sijajua itakuwaje. Kinachoonekana ni kwamba Kocha Phiri si mbaya, ila hana nguvu kwa baadhi ya wachezaji ambao wamepoteza nidhamu.
“Pia amekuwa na tabia ya kutotaka kuwaudhi watu, anataka kila mtu afurahi hata kama anaharibu. Ndiyo maana viongozi wameona vema kumleta Poulsen.”
Iwapo Simba itashikilia msimamo wake wa kumleta Poulsen, basi lazima itaendelea na rekodi yake ya kuwa tim iliyofukuza makocha wengi zaidi kwa misimu mitatu mfululizo.

Katika misimu miwili iliyopita, Simba ilifundishwa na makocha wanne tofauti, kila mmoja akifundisha nusu msimu.
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic