Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya
mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya
Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane.
Katika majina hayo 24, Nooij amemuita beki mkongwe wa zamani wa Yanga, Abuu Mtiro ambaye sasa anakipiga Kagera Sugar.
Akizungumza
Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia
kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku
hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Novemba
11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka
kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka
Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.
Wachezaji
walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias
Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam),
Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani
(Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim
Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao
(Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum
Abubakar (Azam).
Washambuliaji
ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho
Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).
0 COMMENTS:
Post a Comment