Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Wilayani
Temeke, Fortunatus Mang’wela amesema uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) umekuwa ukimuwinga na kumfanyia vituko.
Mang’wela maarufu kama Photu amesema
alizuiwa kuingia Uwanja wa Taifa katika mechi mbili za Ligi Kuu zilizochezwa Jumamosi
na Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam.
“Kisa kikubwa ni kutaka Jamal Malinzi atokea
ufafanuzi kuhusiana na ufujaji wa fedha za TFF katika mkataba wa TBL.
“Dk Ndumbaro amekuwa akizungumza na kutoa
taarifa kuhusiana na ufujaji huo huku akiwa na data za kutosha. Umeona hata TBL
hawajasema lolote, sasa basi Malinzi aseme jambo, hilo ndiyo kosa langu,”
alisema Photu.
“Achana na hivyo, niliitiwa hadi askari
polisi, ni mtu ambaye ninamjua, akaniambia eti nimemtukana (Wilfred) Kidau, hii
ajabu kabisa,” anasema kiongozi huyo maarufu katika eneo la Temeke.
USIKOSE KUSOMA MAKALA YA KIONGOZI HUYO KESHO
AKIELEZEA KWA UNDANI YALIYOMKUTA IKIWA NI PAMOJA NA KUFIKISHWA KUITIWA ASKARI
POLISI AMUONDOE UWANJANI, LAKINI ASKARI WENGINE WAKAONA JAMBO HILO NI KISASI
KISICHO NA SABABU NA KUAMUA KUMUACHIA.
0 COMMENTS:
Post a Comment