Msemaji mwenye maneno mengi wa Masau Bwire
amesema mashabiki wa Simba walimpa wakati mgumu timu yake ya Ruvu Shooting
ilipoivaa Simba Jumapili.
Amesema mashabiki hao walimzunguka na
kumfanya ajikute akimwagija jacho kupindukia, lakini akawasifia kuwa ni
wastaarabu sana.
“Mashabiki wa Simba si kama wale wa Tanga,
maana walinizunguka na kunipa wakati mgumu sana.
“Lakini hawakuwa wakorofi, wengi walitaka
kuniona, kunipa mkono na zaidi walikuwa na utani wakiniuliza nilichosema wala
hakikuwa,” alisema Bwire.
Lakini wale wa Tanga ni hatari sana,
walitaka kunimaliza pale Mkwakwani tena bila sababu za msingi, si watu
wastaarabu hata kidogo.
Mashabiki hao walimzunguka msemaji huyo wa
Ruvu Shooting mara baada ya Simba kuifunga trimu yake kwa bao 1-0 na kuandika
ushindi wa kwanza katika msimu huu baada ya kuwa imecheza mechi sita na kutoka
zote sare.
0 COMMENTS:
Post a Comment