Kikosi
cha wachezaji 23 wa Taifa Stars tayari kimewasili Johannesburg, Afrika Kusini
tayari kwa maandalizi ya mechi dhidi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland.
Mechi
hiyo itafanyika Jumapili (Novemba 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa
Somhlolo jijini Swaziland. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa itakapoondoka kwenda Mbabane.
Wachezaji
wote walioitwa na Kocha Mart Nooij wapo kwenye msafara huo isipokuwa kiungo
mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye amebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya
kifamilia.
Taifa
Stars inatarajia kurejea nyumbani Jumatatu (Novemba 17 mwaka huu) saa 12.45
jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
Wakati
huo huo, kikosi cha maboresho cha Taifa Stars kitacheza mechi ya kirafiki na
timu ya Taifa ya Rwanda kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23. Mechi hiyo
itachezwa Desemba 9 mwaka huu nchini Tanzania.
Kikosi
cha maboresho cha Taifa Stars kinachoundwa na wachezaji wenye umri chini ya
miaka 23 kitakuwa kinakutana mara moja kila mwezi hadi Mei mwakani kwa ajili ya
mazoezi na kucheza mechi moja ya kirafiki.
Kocha
Mart Nooij atatangaza kikosi kwa ajili ya mechi hiyo na programu nzima mara
atakaporejea kutoka Swaziland.
0 COMMENTS:
Post a Comment