Na Baraka Kizuguto (Yanga)
Mabingwa mara
24 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara timu ya Young Africans kesho watashuka dimba la
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kucheza na timu ya Mgambo JKT kutoka
mkoani Tanga katika muendelezo wa michezo ya VPL mzunguko wa nane.
Kocha mkuu wa Young Africans, Marcio Maximo amesema anakiamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo dhidi ya Mgambo JKT na kurudi katika nafasi mbili za juu za msimamo wa Ligi Kuu ya Bara, Jumamosi.
Maximo amesema: "Tumecheza vizuri mechi tatu zilizopita, matokeo ya mechi dhidi ya Kagera Sugar hatukugemea kupoteza mchezo, lakini naamini katika Uwanja wa Taifa tuna nafasi nzuri ya kupata ushindi na kucheza kandanda safi."
Aidha, Maximo amesema wachezaji wote wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Mgambo JKT kesho, nawaheshimu wapinzanii wetu ni wazuri kwa sababu hii ni ligi na kila mmoja anahitaji pointi tatu muhimu tumejiandaa kupata ushindi.
"Nina kikosi kizuri chenye ushindani, kwanza tumeshinda Ngao ya Jamii, pili tunategemea kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na kuingia hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la washindi barani Afrika mwakani," alisema Maximo.
Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mgambo JKT, Kikosi cha Young Africans kimeingia kambini jana jioni katika hoteli ya Valley View kujiandaa na mchezo huo ambapo wa wachezaji wawili Nahodha wa timu Nadir Haroub "Cannavaro" na mshambuliaji Hussein Javu wataukosa mchezo huo.
Kocha Marcio Maximo amewaomba wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans kujitokeza kesho kwa wingi Uwanja wa Taifa kuja kuwapa hamasa vijana na kuwashangilia katika mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment