Mama Tunu Pinda amesema kuna kila sababu kwa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutatua migogoro lukuki na malumbano
yasiyoisha dhidi ya wadau mbalimbali wa soka nchini.
Mke huyo wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
amesema kama TFF haitaliona hilo, basi itakimbiza wadhamini.
“TFF inapaswa kuisaidia serikali kuleta
ustawi wa maendeleo ya michezo nchini. Migogoro haiwezi kuisaidia lolote.
“Kibaya zaidi wanalumbana kuhusiana na fedha
za wadhamini, nani atakuwa tayari kuzipeleka fedha zake zigombaniwe na kuliwa
na wajanja wachache,” alisema Mama Pinda.
Mama Pinda amekuwa si mzungumzaji sana
katika masuala ya michezo lakini safari hii amejitokeza na kuwaasa TFF.
Shirikisho hilo chini ya Jamal Malinzi
limekuwa likiingia kwenye migogoro na wadau wengi wa soka kila kukicha.
Tokea utawala wa Malinzi uingie madarakani,
umekuwa ukifanya timuatimua ya maofisa kadhaa wa shirikisho hilo.
Pia limekuwa likilumbana na wadau mbalimbali
hadharani au chinichini.
SOURCE: NIPASHE
0 COMMENTS:
Post a Comment