Matokeo si mazuri katika kikosi cha Mbeya City katika Ligi Kuu Bara.
Mdhamini wa timu hiyo Bin Slum Tyres Ltd, ameeleza kusikitishwa na mwenendo wa
timu hiyo kwa msimu huu.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Nassor Bin Slum amesema anasikitishwa na kinachotokea
aliyoidhamini Mbeya City ya Mbeya kwa mkataba wenye thamani ya shilingi milioni
300.
“Inasikitisha sana kuona Mbeya City haifanyi vizuri kwani mdhamini
yeyote anafurahi akiona timu anayoidhamini inafanya vizuri. Kufanya vizuri kwa
timu ndipo kunasababisha mashabiki wengi waingie uwanjani na kuifuatilia timu,
hivyo kufanya mdhamini apate faida.
“Iwapo timu inafanya vibaya na watu wakawa hawawafuatilii kwa kupata
habari zao inasababisha mdhamini kutopata faida, inabidi uongozi ukae na
uangalie tatizo lipo wapi na kulekebisha makosa ili timu iweze kurudi katika
kiwango chake,” alisema Bin Slum.
0 COMMENTS:
Post a Comment