TIPPO (KATIKATI) AKIWA NA KOCHA WA KILIMANJARO STARS WAKATI HUO, JAN POULSEN. KULIA NI SLYVETRE MARSH ALIYEKUWA MSAIDIZI NA DAKTARI, MWANANDI JUMA MWANKEMWA. |
Nahodha wa zamani wa Coastal Union, Othmani Tippo ‘Zizzou’
ameishauri timu yake hiyo ya zamani kuhakikisha inamsajili kiungo mmoja namba
nane katika usajili wa dirisha dogo kwenye msimu huu.
Hiyo, ni baada ya kuiona Coastal katika michezo miwili mikubwa dhidi
ya Simba ambayo ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2 kabla ya kuvaana na mabingwa
watetezi wa ligi kuu Azam FC ambao nao walitoka 1-1.
Tippo amesema huo ndiyo upungufu aliouona katika kikosi hicho
kinachonolewa na Mkenya, Yusuf Chippo, akisaidiana na Benard ‘Ben’ Mwalala.
Tippo alisema, anaamini kama timu hiyo ikifanikiwa kumpata kiungo
mwenye uwezo mkubwa atakayesaidiana na Razack Khalfan kwenye usajili huo
unaotarajiwa kufunguliwa kesho Jumamosi basi itafanya vizuri msimu huu.
“Nimeiangalia Coastal Union katika mechi dhidi ya Simba na Azam FC,
walionyesha soka safi sana.
“Kikubwa wanachotakiwa kukifanya ni kusajili kiungo mmoja
mchezeshaji,” alisema Tippo anayemiliki maduka ya vifaa vya michezo nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment