Beki wa Simba, Joram Mgeveke hafurahii maisha ya kubaki benchi tokea
alipotua Msimbazi akitokea Lipuli FC ya Iringa, mwanzoni mwa msimu huu na
tayari ameanza kufikiria kuhamisha makazi.
Mlezi wa Lipuli FC, Cpryan Gwivaha amekiri kutafutwa na Mgeveke
kuhusu kutaka kuondoka Simba lakini akamsihi abaki, ipo siku anaweza kupata
namba.
“Mgeveke ameniambia mara kadhaa kuwa ni bora aondoke maana anaona
kipaji chake kinakufa, amekuwa ni mtu wa benchi na ikumbukwe bado ni kijana mdogo,
nimemwambia ajitahidi mazoezini ipo siku kocha atamkubali,” alisema Gwivaha.
Alipoulizwa Katibu wa
Simba, Stephene Ally, juu ya suala hilo alisema kuwa suala la mchezaji kuondoka
litatokana na mahitaji ya kocha.
0 COMMENTS:
Post a Comment