Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara,
Azam FC, wamepokea vipigo viwili mfululizo lakini wamesema: “Hatujakata tamaa
ya ubingwa.”
Wiki mbili zilizopita, Azam walikuwa
wanaongoza msimamo wa ligi lakini sasa wameporomoka mpaka nafasi ya tatu
kufuatia vipigo dhidi ya JKT Ruvu na Ndanda, juzi.
Azam FC ilichapwa bao 1-0 na wenyeji
wake Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Kabla ilikuwa
imepoteza mechi nyingi dhidi ya JKT Ruvu.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jafar Idd,
amesema ligi bado.
Jafar amesema bado wana kikosi kizuri
na chenye uwezo wa kupambana kwa ajili ya kutetea ubingwa wake na kwa sasa
wanajipanga kusahihisha makosa waliyoyafanya kwenye michezo hiyo.
“Tumekubali kuwa tumepoteza michezo
yetu hiyo miwili lakini bado hatujakata tamaa ya kutetea ubingwa wetu kwani kwa
sasa tunajipanga kuangalia wapi tulikosea ili kurekebisha makosa hayo na
kufanya vizuri katika michezo ijayo,” alisema Jafar.
0 COMMENTS:
Post a Comment